Habari za Punde

KIPANGA INAKUJA KIVYENGINE MSIMU HUU, YAACHA WACHEZAJI 8 NA KUSAINI 8

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Baada ya msimu ulopita chupuchupu kunusurika kushuka daraja timu ya Kipanga imejipanga upya kuhakikisha msimu huu inafanya vizuri katika ligi kuu soka ya Zanzibar ambayo inatarajiwa kuanza rasmi Oktoba 1,2017.

Akizungumza kwa kujiamini mwenyekiti wa timu ya Kipanga Said Ali Juma Shamhuna amesema timu yake imesajili wachezaji wapya 8 na kuwaacha 8 ambapo kwasasa ameshafunga usajili baada ya kusajili makinda hao huku akiamini msimu huu watafanya vizuri.

“Tumesajili wachezaji 8 wapya na tumewaacha 8, hawa tulosajili wote ni vijana wakitokea Central na daraja la pili, kati ya hao 8 wapya wanne ni askari na wanne ni raia naamini msimu huu tutafanya vizuri sana, wachezaji niliowasajili ni Yahya anatokea Muembeladu, Ibrahim maarufu Deco anatokea Bububu, Benzema anatokea Medson na Cheda pia anatokea Medson hao ni wachezaji raia lakini wachezaji Majeshi nilioongeza ni Moko, Ahmada, Ali Mohd na Ali Bashir”. Alisema Shamhuna.

Msimu uliopita Kipanga bado kidogo ishuke daraja baada ya kuwa na alama sawa na timu ya Malindi iliyoshuka daraja wote wamemaliza ligi na alama 42 lakini Kipanga apata faida ya mabao ya akiba baada ya kuwa na akiba ya mabao 4 huku wenzao Malindi walikuwa na deni la mabao 7 na kusababisha kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.