Habari za Punde

PRISONS YAMALIZA KAMBI VISIWANI ZANZIBAR KWA KUSHINDA MICHEZO 4 NA SARE 1 DHIDI YA BLACK SAILORSNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu ya Tanzania Prisons ambayo imeweka kambi visiwani Zanzibar imemaliza michezo yake ya kutest mitambo baada ya kuifumua Mlandege kwa mabao 4-1 kwenye mchezo uliopigwa jana saa 2 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Mabao ya Prisons yamefungwa na Lambati Sabiyanka dakika ya 8 na 40, Leunsi Mutalema dakika ya 62 na Eliuti Mpepo dakika ya 84 huku bao pekee la Mlandege likifungwa na Abubakar Ame “Luiz” dakika ya 54.

Prisons iliweka Kambi Visiwani hapa tangu Jumamosi ya Agost 12, 2017 ambapo ilicheza michezo ya kirafiki 5 na kushinda michezo 4 huku mchezo 1 wakitoka sare na Black Sailors ambapo walizifunga timu ya Mlandege, Ngome, KMKM na Dula Boys.

Leo watasafiri na majira ya saa 3 asubuhi kwa kurudi Dar es salaam huku wakiwashukuru wapenz wote wa mpira hapa zanzibar na kushukuru uongozi wa ZFA kwa kuwatafutia timu ambazo zimewapa mazoezi makubwa.

Prisons ambayo inafundishwa na kocha Mzanzibar Abdallah Mohd “Bares” iliweka kambi visiwani hapa kwa kujiandaa na ligi kuu soka ya Tanzania bara msimu mpya ambapo mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo watacheza Jumamosi Agost 26, 2017 dhidi ya timu mpya iliyopanda daraja ya Njombe Mji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.