Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambe ni mgombea mteule wa nafasi ya uwakilishi jimbo la kiwani Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema atahakikisha anaitekeleza kwa vitendo ilani ya chama cha mapinduzi pindi akichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo hilo.
Ameyasema hayo mara baada ya kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombe nafasi ya uwakilishi Jimbo la kiwani katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba.
Ndugu Hemed amesema kuwa ilani ya chama ndio muongozo kwa wagombea wote wa CCM hivyo atahakikisha anaifuata vyema pamoja na kuwatekelezea wananchi mahitaji yao ya lazima ndani ya jimbo la kiwani ikiwemo kuwapatia huduma ya maji safi na salama huduma za afya, elimu na miundombinu.
Amesema pindi akipata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa muwakilishi wa jimbo la Kiwani atahakikisha anawatumikia wanakiwani wote kwa usawa bila ya kujali itikadi zao kama chama cha mapinduzi kinavyoelekeza.
Amesema ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2025- 2030 imegawiwa kimikoa hivyo wananchi wa mikoa yote ya Zanzibar watanufaika na kupata maendeleo bila ya kujaali dini, jinsia au kabila.
Sambamba na hayo ameendelea kuwakumbusha wanasiasa wote kuhakikisha wanayatumia majukwaa ya kisiasa kwa kuhubiri amani na mshikamamano na kukumbuka kuwa wazanzibari wote ni ndugu na kuna maisha baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR )
Tarehe 08.09.2025
No comments:
Post a Comment