Habari za Punde

Waandhishi Watakiwa Kuwa Waangalifu Katika Kuandika Habari za Uchaguzi Ili Kuepusha Uchochezi na Uvunjifu wa Amani Katika Kipindi Chote cha Uchaguzi Mkuu

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe.Jaji George Joseph Kazi akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano na Wadau wa Habari Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Maisara Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 8-9-2025.


Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwa waangalifu katika  kuandika Habari za Uchaguzi ili kuepusha uchochezi na uvunjifu wa Amani  katika kipindi Chote Uchaguzi Mkuu unayotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji George  Joseph Kazi katika Ukumbi wa Tume hiyo Maisara  katika Mafunzo ya wadau wa habari wa Uchaguzi Mkuu
Amesema kuwa lugha ya mwandishi inaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani au ni yenye kudumisha Amani hivyo ni vyema kuzingatia  maadili, haki na wajibu katika kazi zao

Ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni matayarisho ya kuelekea Uchaguzi Mkuu ambapo waandishi wa habari wanatakiwa kutambua Sheria na kanuni katika kuandika habari za Uchaguzi

Aidha amewashukuru wanahabari kwa kuwapatia wananchi taarifa za Tume ya Uchaguzi muda wote kuanzia uwandikishaji wa daftari la wapiga kura hadi kufikia sasa

Akitoa taarifa kuhusu matayarisho ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025 Mkurugenzi wa Tume hiyo Thabit Idarus Faina amesema wadau wa Uchaguzi wana haki na Wajibu wa kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa salama na Amani.

 Aidha ameeleza kuwa huo ni Uchaguzi wa saba tangu kuanza kufanyika mwaka 1992 kuanza kwa mifumo wa vyama vingi  ambapo kila unapomaliza uchaguzi mmoja Tume inaandaa matayarisho ya Uchaguzi mwengine

Akiwasilisha  Wajibu na Maadili ya waandishi wa Habari wakati wa Uchaguzi  Kaimu Mkurugenzi wa Habari Maelezo Asha Abdi Makame amesema kuwa muandishi ana wajibu kufuatilia na kuripoti Kampeni kwa usawa pamoja na kutoa fursa sawa kwa wagombea wa vyama vyote bila ya upendeleo.

Nao wadau wa Uchaguzi wameiomba Tume ya Uchaguzi na Tume ya Utangazaji Zanzibar kushirikiana na Jeshi la polisi ili kufanya kazi zao kwa ufanisi bila ya usumbufu wowote.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Thabit Idarous Faina akionesha Kikoti kitakacho tumiwa na Waandishi wa Habari watakaoripoti Habari za Uchaguzi katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Idrissa Haji Jecha akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Mwandishi wa Habari kutoka Alfatah Tv Online Rashid Salum Mohamed akiuliza maswali katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Mwanasheria wa Tme ya Utangazaji Zanzibar Khadija Mabrouk Hassan akiwasilisha mada kuhusiana na Kanuni ya Huduma za Utangazajiwakati wa Uchaguzi katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Mkuu wa Kurugenzi ya Elimu ya Wapiga Kura na Mawasiliano kwa Umma Juma Msanifu Sheha akiwasilisha mada kuhusiana na Mwongozo kwa Vyombo vya Habari vya Umma katika kutangaza Kampeni za wagombea katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Mhariri wa Habari TBC Zanzibar Nassra Khatib akiuliza maswali katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Asha Abdi Makame akiwasilisha mada kuhusiana na Maadili ya Waandishi wa Habari wakati wa Uchaguzi katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Wadau wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.08/09/2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.