AFISA
Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan
Amour Mohamed, akiwaonyesha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar kushoto, washiriki wa mafunzo ya
utayarishaji wa katiba na sheria, ambao ni viongozi wa dini, asasi za kirai,
wanajamii na watu maarufu, mafunzo hayo ya siku mbili, yalifanyika skuli ya
Maandalizi Madungu Chakechake Pemba
MWANASHERIA Dhamana kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka
Pemba, ‘DPP’ Ali Rajab Ali, akiidadavua sheria mpya ya ushahidi ya Zanzibar no
9 ya mwaka 2016, kwa viongozi wa dini, asasi za kirai, wanajamii na watu
maarufu, kwenye mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria, yaliofanyika skuli
ya Maandalizi Madungu Chakechake, na kutayarishwa na ZLSC tawi la Pemba
AFISA
Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan
Amour Mohamed, akitoa mada ya utayarishaji wa katiba na sheria, kwa viongozi wa
dini, asasi za kirai, wanajamii na watu maarufu, mafunzo hayo ya siku mbili, yalifanyika
skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake Pemba
WASHIRIKI wa
mafunzo ya utayarishaji wa katiba na sheria, ambao ni viongozi wa dini, asasi
za kirai, wanajamii na watu maarufu, kisiwani Pemba wakifuatilia mafunzo hayo
ya siku mbili yaliofanyika skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake na kuandaliwa
na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment