Habari za Punde

Mradi wa Best of Zanzibar Unaotowa Masomo ya Ziada ya Elimu kwa Watoto wa Kijiji cha Mbuyu Tende na Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja

Mkurugenzi Elimu Msingi na Maandalizi Bi Sofia Rijali akizungumza na Wananchi wa Vijiji vya Mbuyu Tende na Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Wilaya Kaskazini A, akitoa nasaha zake kwa wananchi hao kuwahimiza watoto wao kama kupata masomo ya ziara ya masomo ya Hesabati na Kingereza yanayotolewa kupitia Mradi wa Best Of Zanzibar kuinua viwango vya elimu kwa watoto ho wa vijiji hivyo ili kuweza kufanya vizuri katika masomo yao darasani na katika mitihani yao. Mradi huo unaosimamiwa na Kampuni ya ujenzi wa Hoteli ya Kitalii Matemwe ya PennyRoyal. jumla ya watoto 400 wananufaika na mradi huo ya masomo ya ziada. 
Wazazi na wananchi wa Watoto wa Skuli za Msingi na Sekondari za Mbuyu Tende na Kijiji wanaopata masomo ya ziara ya Hisabati na Kiingereza wakimsikiliza Mkurugenzi wa Elimu Msingi na Maandalizi alipokuwa akitowa nasaha zake kwao.
Mratibi wa Mradi wa Elimu ya Best of Zanzibar Ali Hamadi akizungumza wakati wa mkutano huo na wazazi wa Watoto wa Skuli ya Mbuyu Tende na Kijini wanaopata masomo ya ziada ya Hesabati na Kiingereza na kuwataka wazazi hao kuwasajihisha watoto wao kuhudhuria masomo hayo ya ziara yanayotolewa wakati wa saa za kumaliza masomno yao ya kawaidi kuhudhuria kwa wingi ili kuweza kuinua kiwango chao cha ufahamu wa masomo yao wakiwa darasani.

Mratibu wa Mradi wa Best of Zanzibar Elimu ya Afya na Mazingira Nahiya akizungumza wakati wa mkutano huo na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi na Maandalizi Bi Sofia Rijali, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Wananchi wa Vijini vya Mbuyu Tende na Kijini wakifuatilia mkutano huo wakiwa katika viwanja vya Skuli ya Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja. 
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari na Msingi Kijini Matemwe akionesha kanuni ya kuaza kwa masomo ya awali kwa watoto wakati wa mkutano huo na Mkurugenzi Elimu ya Msingi na Maandalizi Unguja Bi Sofia Rijali mkutano uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Kijini.  
Wazazi wakifuatilia mkutano huo wa kuwahamasisha kuwahimiza Watoto wao kuhudhuria Elimu ya Masomo ya ziada ya Hesabati na Kiingereza yanayotoilewa na Mradi wa Best of Zanzibar ulioko chini ya Kampuni ya ujenzi wa Hoteli ya Kitalii ya Penny Royal Zanzibar.
Kiongozi wa Kamati ya Maendeleo Kijiji cha Kijini akichangia wakati wa mkutano huo na Mkurugenzi wa Elimu Msingi na Maandalizi kuhamasisha wazazi kutowa fursa ya watoto wao kupata elimu ya masomo ya ziada yanayotolewa na Mradi wa Best of Zanzibar.   
Wzazi wakichangia wakati wa mkutano huo kutowa fursa kwa wanafunzi wa Skuli za Mbuyu Tende na Kijini Matemwe.
Mzazi akisisitiza jambo wakati akichangia katika mkutano huo uliowashirikisha Wazazi wa Watoto wa Skuli za Mbuyu Tende na Kijini Wilaya ya Kaskazini A Unguja wanaopata masomo ya ziada ya Hisabati na Kiingereza yanayotolea kupitia mpongo wa Mradi wa Best of Zanzibar, ulioko chini ya kampuni ya ujenzi wa kijiji cha Kitalii Matemwe Penny Royal. 
Wananchi wa Watoto wa Skuli za Mbuyu Tende na Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakifuatilia mkutano huo ulinaofanyika katika viwanja vya skuli ya sekondari na msingi kijini matemwe Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.