Habari za Punde

DAU NA JAFFAR WAULA ZFA, WACHUKUA NAFASI YA HUSSEIN NA ATTAI WALIOFUKUZWA NA MKUTANO MKUU

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kamati Tendaji ya ZFA Wilaya ya Mjini imemteuwa Abdul-Wahab Dau Haji kuwa mjumbe wa Wilaya hiyo kuwakilisha ZFA Taifa baada ya kujaza nafasi tupu iliyoachwa na Hussein Ali Ahmada.

Akithibitisha kupokea barua ya uteuzi huo Dau amekiri kuteuliwa kuchukua nafasi hiyo huku akihimiza ushirikiano ili wafanye kazi kwa ufanisi ndani ya ZFA.

"Ni kweli jana nimepokea barua ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa ZFA Wilaya ya Mjini kuwakilisha ZFA Taifa, nashkuru kwa kuniamini mpaka wakaniteuwa, kubwa naomba ushirikiano ili tufanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu". Alisema Dau.

Wakati huo huo pia ZFA Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja wamemteuwa Jaffar Ali Haji kuwa Mjumbe wa Wilaya hiyo kwenda kuwakilisha ZFA Taifa ambapo amejaza nafasi tupu iliyoachwa na  Massoud Attai.

Wajumbe hao wawili wanachukua nafasi tupu zilizoachwa na Hussen Ali Ahmada kutoka Wilaya ya Mjini na Massoud Attai wa Kaskazini "A" Unguja ambao walifungiwa maisha kutojihusisha na Soka kutokana na sababu tofauti baada ya Mkutano Mkuu wa dharura ZFA Taifa kuwafukuza, Mkutano ambao uliofanyika April 22, 2017 katika Ukumbi wa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.