Habari za Punde

Yaliojiri Viwanja Vya Fumba Baraza la Eid Al Hajj

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akipokea heshima ya gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid Al Hajj Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Kikosi cha FFU wakitowa heshima kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al Hajj Dk Ali Mohamed Shein, baada ya kumaliza kulihutubia Baraza la Eid Al Hajj katika viwanja vya Fumba Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al Hajj Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud na Meya wa Manispa ya Magharibi Unguja wakielekea katika viwanja vya hafla hiyo kupata dhifa baada ya kumalizika kwa baraza la eid al hajj. 
Makamu wa Rais Mstaaf Dk Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Waziri wa Sheria Katiba na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman katika viwanja vya fumba baada ya kumalizika kwa Baraza la Kitaifa la Eid Al Hajj lililofanyika katika maeneo huru ya Uchumi Fumba Zanzibar. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.