Habari za Punde

Black Sailors yazidi kung'ara, Charawe kama Miembeni City


 Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena jana kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo saa 8 za mchana Black Sailors (Mabaharia Weusi) waliitandika Kilimani City mabao 2-0.

Mabao ya Sailors yamefungwa na Hassan Said dakika ya 1 na Hassan Mkwabi dakika ya 89 kwa mkwaju wa penalty baada ya mlinzi wa City Azizi Shaweji kumfanyia mazambi Iddi Idrissa.

Pia katika mchezo huo mchezaji wa Kilimani City Humud Suleiman ameonyeshwa kadi nyekundu.
Saa 10 za jioni Mabaharia wa KMKM wakafanikiwa kuitandika Charawe mabao 2-0.

Mabao ya KMKM yamefungwa na Salum Akida dakika ya 60 na Mudrik Muhibu dakika ya 66.

Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo Saa 8:00 za mchana Zimamoto dhidi ya Kipanga na saa 10:00 za jioni Polisi na KVZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.