Habari za Punde

Wanafunzi watakiwa kujitenga na matumizi ya simu na TV yasiyo sahihi

Na Binagi Media Group
Shule za Eden ni za kutwa na bweni zikijumuisha shule ya Awali, Msingi na Sekondari zilizopo Jijini Mwanza.

Katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu, wanafunzi wote wa Eden wamefaulu mtihani wao kwa kiwango cha juu na kuwa miongoni mwa shule tatu bora mkoani Mwanza zilizofanya vizuri.

Jana Oktoba 21,2017 ilikuwa siku ya Mahafali ya saba ya shule ya Sekondari Eden iliyopo Mandu Kata ya Nyakato Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza ambapo Meneja wa Shule za Eden anaeleza ubora wa shule hizo.

Wahitimu wa shule ya sekondari Eden iliyopo Mandu Kata ya Nyakato Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza wakiwa kwenye mahafali ya saba ya shule hiyo jana
Mkurugenzi wa shule za Eden, Joseph Mbabazi aliwataka wanafunzi kuzingatia maadili mema waliyofundishwa shuleni hapo wakati na baada ya mtihani wao wa kidato cha nne hatua ambayo itawaepusha na vishawishi na hivyo kutimiza ndoto yao kimasomo. Aidha aliwahisi pia wazazi na walezi kuzingatia malezi bora kwa watoto wao
Meneja wa shule za Eden, Mwl.Charllote Mbabazi akizungumza kwenye mahafali hayo
Mgeni rasmi, Mdhibiti wa ubora wa shule Kanda ya Ziwa Michael Cheyo, akizungumza kwenye mahafali hayo
Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri shuleni hapo wakipokea zawadi
Mgeni rasmi akipokea zawdi kutoka kwa Mkurugenzi wa shule za Eden
Mgeni rasmi akisalimiana na Mkuu wa shule ya sekondari Eden
Wahitimu wa shule ya sekondari Eden wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi
Meza Kuu
Wahitimu wa Eden sekondari wakionyesha michezo mbalimbali
Bonyeza HAPA kutazama picha zaidi za mahafali

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.