Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Atuma Salamu za Pongezi Kwa Rais wa Zambia.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                                            23.10.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Changwa Lungu kwa kutimiza miaka 53 tokea Taifa hilo kupata uhuru wake.

Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana pamoja na ndugu zao wa Zambia katika kusherehekea siku hii muhimu katika historia ya nchi hiyo ambapo tukio hili la kihistoria lilitokea Oktoba 24 mwaka 1964 ambapo Zambia ilipata uhuru kutoka koloni la Kiengereza.

Aidha, salamu hizo, zilieleza kuwa tukio hilo kubwa, linatoa nafasi ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa kati ya nchi mbili hizo hatua ambayo itaimarisha zaidi uhusiano katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa yakiwemo mashirikiano ndani ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Jumuiya nyenginezo za Maendeleo.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Zambia, afya njema na kuwatakia sherehe njema zenye amani na utulivu wananchi wa nchi hiyo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.