Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Simba Kikiwasili Kisiwani Zanzibar Kwa Boti ya Kampuni ya Azam Kilimanjaro V Asubuhi Hii Kwa Ajili ya Kambi Yao.

Mshambuliaji wa Timu ya Simba Kichuya akiwasili katika bandari ya Zanzibar na Timu yake ikiwa na Wachezaji na Viongozi 24 kwa ajili ya Kambi ya mazoezi yao kwa kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania kupambana na watani wao Timu ya Yanga jumamosi ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Timu hiyo imewasili asubuhi kwa boti ya Kilimanjaro V ikitokea Jijini Dar es Salaam.  
Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Omog akiwasili katika bandari ya Zanzibar akiwa na wachezaji wake kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao na Timu ya Yanga African jumamosi. 


Kiongozi wa Timu ya Simba Tawi la Zanzibar Mshangama akiwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Omog alipowasili katika bandari ya Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao na Timu ya Yanga African Jijini Da es Salaam mwishoni mwa wiki hii.

Wachezaji wa Timu ya Simba wakiwa katika basi baada ya kuwasili Zanzibar na kuelekea katika Kambi yao waliopangia kwa ajili ya kuaza mazoezi leo jioni katika uwanja wa chunga fuoni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.