Habari za Punde

Dakika za Majeruhi Zailiza Timu ya Miembeni City kwa Kipigo Cha Bao 1-0 Dhidi ya Polisi Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Miembeni City leo imekaribishwa kwenye ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kuchapwa bao 1-0 na Polisi mchezo uliochezwa saa 10 za jioni kwenye uwanja wa Amaan.

Bao pekee la Polisi lililopeleka msiba kwa City limefungwa na Abdallah Omar dakika ya 90 ya mchezo huo.

Ligi hiyo itaendelea tena leo saa 1:00 za usiku kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Zimamoto.

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utakamilika kesho kwa kupigwa mchezo mmoja saa 10:00 za jioni kati ya Black Sailors dhidi ya Chuoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.