Habari za Punde

Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto Zanzibar Chafanikiwa Kuudhibiti Moto Katika Kituo cha Kusambaza Umeme Marikiti Darajani.

Askari wa Kikosi cha Uokozi na Zimamoto Zanzibar wakiwa nje ya kibanda cha Transfoma ya kusambaza umeme katika maeneo ya mitaa ya mji mkongwe baada ya kutokea hitilafu na kuripuka kutokana na hitilafu hiyo kwa juhudi zao Kikosi hicho wameweza kuudhibiti moto huo na kuuzima kabla ya kuleta madhara kwa maeneo ya jirani na eneo hilo. Katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Fundi wa Shirika la Umeme Zanzibar akiwa na Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji baada ya zoezi hilo kumalizika la uzimaji wa moto huo. 


Wananchi wakiangalia zoezi hilo la uzimaji wa moto wakiwa kanda ya barabara katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.