Habari za Punde

TAIFA YA JANG’OMBE MAMBO BADO MECHI NNE HAWAJAONJA LADHA YA USHINDI, KVZ NA MAFUNZO WALA SAHANI MOJA, KESHO KMKM NA ZIMAMOTO

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Jang’ombe (Wakombozi wa Ngambo) imeendelea kucheza pasipo kupata ushindi katika michezo yake ya ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya leo saa 8 za mchana kutoka sare ya 0-0 dhidi ya JKU katika uwanja wa Amaan.

Kwa matokeo hayo Taifa imefikisha alama 3 kufuatia kufungwa mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitatu wakati JKU amejikusanyia alama 10 baada ya kushinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja.

Saa 10 za jioni ulipigwa mchezo mwengine katika uwanja wa Amaan kati ya KVZ na Mafunzo mchezo ambao umemalizika kwa sare ya 0-0.

KVZ anaongoza ligi hiyo akifuatiwa na JKU baada ya timu zote hizo kuwa na alama 10 katika michezo yao 4 waliyocheza huku Mafunzo baada ya mechi ya leo amefikisha alama 5 kufutia kushinda mmoja, sare 2 na kufungwa mmoja.

Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.

Saa 8:00 za mchana wataanza Wana Jeshi timu ya Kipanga kukupiga na Maafande wa Polisi na saa 10:00 za jioni watachuwana kati ya KMKM dhidi ya Zimamoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.