Habari za Punde

Tawi la Yanga Amaan Zanzibar Kufanya Mkutano leo Jumapili.

Na: Abubakar Khatib, Unguja.
Msemaji wa Tawi la Yanga la Amaan Mjini Unguja, Maulid Omar Mpili amewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mkutano maalum unaotarajiwa kufanyika Oktoba 15, Jumapili kwenye shule ya Msingi Nyerere kuanzia saa 4:00 za asubuhi.
Akizungumza na Mtandao huu Mpili amesema kuwa wanachama wote wajitokeze siku hiyo kwa kujadili timu yao ambayo kwasasa inaonekana kutokuwa sawa hasa katika safu ya ushambuliaji.
Amesema lengo ni kukaa pamoja na kujua nini wafanye ili timu yao iendelee kutwaa taji la ligi kuu soka Tanzania bara kwa mara ya 4 mfululizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.