Habari za Punde

ZIMAMOTO YAPIGWA NNE,SONGORO APIGA HAT-TRICK YA KWANZA MSIMU HUU ZENJ

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Mshambuliaji wa KVZ Salum Songoro amefungua ukurasa mpya ligi kuu soka ya Zanzibar msimu huu baada kufunga hat-trick ya kwanza katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Zimamoto mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan.

Songoro alifunga bao hizo katika dakika ya 9, 16 na 42, Sultan Juma Kaskas alifunga bao la nne katika dakika ya 61 huku mabao ya Zimamoto yalifungwa na Nyange Othman Denge dakika ya 63 na Idrissa Simai dakika ya 88.

Mapema saa 8 za mchana Taifa ya Jang’ombe na Polisi walishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika uwanja wa Amaan.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumanne 17/10/2017 saa 8:00 za mchana Kipanga vs Charawe na saa 10:00 za jioni KMKM vs Kilimani City. 
Jumatano 18/10/2017 saa 10:00 za jioni Black Sailors vs Jang’ombe Boys.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.