Habari za Punde

ZLSC Yawataka Vijana Kujifunza Sheria za Nchi.

Na. Salmin Juma - Pemba
Afisa Mipango  wa kituo cha huduma za sheria tawi la Pemba Khalfan Amour amewataka vijana nchini wawe na utamaduni wa kujifunza sheria za nchi kwani kufanya hivyo kutawaongoza katika kufanya majumuku yao vizuri na pia itakua dira ya maendeleo katika maisha yao.

Ameyasema hayo leo huko katika ukumbi wa kituo cha huduma za sheria ZLSC upande wa Pemba maeneo ya  chakechake mjini alipokua akingumza na vijana wa mkoa wa kusini Pemba katika kikao maalumu  cha tathmini juu ya mafunzo mbalimbali ya taratibu za uwandaaji  wa katiba na sheria tofauti za nchi kupitia mafunzo waliyowahi kuwapa vijana hao.

Khalfan alisema , kutokana na mafunzo waliyowapatia vijana wa mikoa yote miwili ya Pemba yameonysha mabadiliko makubwa kwao na hata jamii zao kwa mujibu wa maelezo ya vijana wenyewe.

"hali inaonekana tofauti, awali vijana hawa walikua hawana uwelewa wa sheria, kama vile sheria ya mabaraza ya vijana , sheria nambaro 16 ,2013 ambayo moja kwa moja sheria hii  inahusiana na vijana wenyewe, wengine waliingia katika mabaraza ya viajana ilhali hawajui lolote, lakini hivi sasa inaonekana wamepata mwamko na uwelewa wa sheria mbalimbali" alisema Khalfan

Mmoja miongoni mwa washiriki katika kikao hicho ,  Mohd Khamis Suleiman kutokea Mahuduthi Kengeja alisema, anakishukuru  sana kituo cha huduma za sheria Pemba kwa msaada wao wa kuwajuza masuala ya kisheria kwani hivi sasa  amepata kujua sheria mbalimbali za nchi pamoja na kuijua katiba yake inayoongoza nchini.

Alisema , mara baada ya kupata taaluma hiyo aliamua kwenda kijijini kwake kuwafikishia vijana wengine taaluma hiyo , ingawa alipata changamoto kadhaa zilizokua zikimkwaza ikiwamo  suala zima la siasa lakini hakukubali kuyumba na angali anaendelea kutoa taaluma hiyo na wanachi wanaindelea kukubali.

Alisema changamoyo anazokabilaiana nazo , wananchi wengi wao wanachanganya mambo ya sheria na siasa  "unapokwenda kuwaelekeza vijana ili wawe na mwamko katika sheria, wanasema nyinyi ni CCM  tu , kidogo inarejesha nyuma" alisema Suleiman.

Zuwena Nassor Salim kutoka chambani, kwa upande wake alisema , amefurahishwa  na utaratibu wa kituo cha ZLSC  kuwajali vijana kwa kuwapatia taaluma hiyo ya kisheria kwani pia imemsaidia kujua sheria za nchi katika katiba pamoja na kuelewa umuhimu wa vijana kujiunga na mabaraza ya vijana.

Kupitia uwelewa wa kisheria aliyoupata kutoka ZLSC  Salim alisema, aliamua kwenda kushajihisha vijana na wezee katika kijiji chake ili waone umuhimu wa vijana kujiunga na mabaraza hayo  na alichokigundua ni kuwa, bado wananchi wana uwelewa mdogo wa sheria kwani wengi miongoni mwao wanaamini mabaraza ya vijana ni maalumu  kwa watu wasiokua na heshima
" ukiwashajihisha wajiunge katika baraza la vijana wanasema ni mabaraza ya watovu wa adabu" alisema Salim.

Aidha aliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya wananchi  kijijini kwao wanaitikadi kuwa kujiunga na mabaraza ya vijana ni kuisadia CCM kura za ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2020 jambo ambalo alipinga na kusema si kweli bali mabaraza ya vijana ni maalum kwa lengo la kuwatafutia njia mbadala vijana ya kufikia maendeleo katika maisha yao.

Katika hatua nyengine alisema , ingawa changamoto hizo zipo lakini anaendelea kupambana nazo na hali inaonekana kubadilika na wengi miongoni mwa wananchi wanaonekana kuwa waelewa.

Kwa Upande wake mwanafunzi kutoka katika skuli ya Connecting Continental Secondry School ambae pia aliwahi kupokea mafunzo ya sheria kupitia ZLSC Pemba Intisar Ahmed Saleh  alisema kutokana na uwelewa wa sheria aliyonao, linapotokeza tatizo la kisheria kwa upande wake anajua wapo pakuelekea.

Alisema, watu vijijini  na wananchi kwa ujumla wengi wao hawana uwelewa wa kutosha katika mambo ya kisheria hivyo kwa makusudi aliamua kuwaita wanafaunzi wenzake na kuanza kuwashajihisha kupenda kujua sheria pamoja na kuwafundisha kile alichokipata kutoka katika kituo hicho na kwa kiwango kikubwa wamekubaliana na uwamuzi huo.

Kituo cha huduma za sheria ZLSC upande wa Pemba kimekua kikishuhudiwa kutoa mafunzo ya kesheria ikiwamo haki za binaadamu, katika na nyenginezo kwa kada tofauti  kama vile askari , walimu, wanafunzi, masheha na mashehe, vijana na wengineyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.