AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango
Pemba,Ibrahim Saleh Juma akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo la Wizara tatu huko
Gombani, kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza
la wawakilishi, wakati walipotembelea kuangalia ujenzi wa jengo hilo
lilipofikia.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
MSIMAMIZI wa Ujenzi wa jengo la Gorofa tatu
linaloendelea kujengwa Gombani, Mbarouk Juma Mbarouk akitoa ufafanuzi kwa
Makamu Menyekiti wa kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar wakati ilipotembelea jengo hilo.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WAJUMBE wa kamati ya Fedha biashara na Kilimo ya
baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakirudia kukagua ujenzi wa jengo la Wizara
tatu linalojengwa Gombani Chake Chake Pemba.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MAKAMU mwenyekiti wa kamati ya Fedha Biashara na
Kilimo ya Baraza la wawakilishi Zanzibar, Hamida Abdalla Issa akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kamati yake kutembelea na kuangalia ujenzi wa
jengo la Gorofa Tatu linalojengwa Gombani Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment