Habari za Punde

Waziri Aboud Afanya Ziara Kisiwani Pemba Kutembelea Miradi Maendeleo.

AFISA Mdhamini wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba, Sihaba Haji Vuai, akimueleza jambo Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Mhe: Mohamed Aboud Mohamed, wakati waziri huyo, alipolitembelea shamba la serikali la Makuwe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake kisiwani Pemba
WAZIRI wa nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Mhe: Mohamed Aboud Mohamed, akielezea namna bora ya kuliimarisha shamba la serikali la Makuwe, wakati waziri huyo alipotembelea shamba hilo
MKUU wa Idara ya Misitu Pemba Said Juma Ali, akizungumza na waziri wa nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Mhe: Mohamed Aboud Mohamed, wakati waziri huyo alipolitembelea shamba la serikali la Makuwe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake kisiwani Pemba
MASANDUKU maalum ya kutegea nyuki yanayomilikiwa na wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba, yaliopo kwenye shamba la serikali la mikarafuu la Makuwe, ambapo shamba hilo kwa sasa linatarajiwa kupandwa upya baadhi ya miti ikiwemo mikarafuu
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa rais Zanzibar Mhe: Mohamed Aboud Mohamed akitembelea sehemu mbali mbali za shamba la serikali la Makuwe, ikiwa ni sehemu ya zaira yake kisiwani Pemba 
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa rais Zanzibar Mhe: Mohamed Aboud Mohamed akitembelea sehemu mbali mbali za shamba la serikali la Makuwe, ikiwa ni sehemu ya zaira yake kisiwani Pemba (Picha na Haji Nassor, Pemba).   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.