Habari za Punde

Zantel Yazindua Kifurushi Maalumu Kwa Watalii Zanzibar.

Zantel kwa mara ya kwanza imezindua huduma ya laini ya simcard ya kwanza nchini maalum kwa watalii ambayo itakuwa na vifurushi vya muda wa maongezi vya kimataifa, kitaifa na bando maalum ya data kilichopewa jina la 'Tourist Pack'.
Laini hizo mpya zitawawezesha wageni wanaokuja Tanzania, kupiga simu za ndani na nje ya nchi katika nchi sita za Ulaya ambazo ni Uingereza, Uhispania, Denmark, Italia, Ufaransa na Marekani kwa bei nafuu zaidi.
Akizindua bidhaa hiyo maalumu katika mkutano na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa alisema laini hizo za malipo ya kabla ambacho zimewalenga zaidi watalii zitakua na ofa ya dakika za kupiga simu za kimataifa na za  hapa nchini ikiwa ni pamoja na kifurushi cha intaneti ndani ya mwezi mmoja.
Aliongeza kuwa nia ya bidhaa hiyo ni kuwasaidia watalii kurahisisha mawasiliano na marafiki, ndugu au familia zao pindi wanapotua chini.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo alisema, Zantel imeamua kuja na laini hizo maalum kwa ajili ya watalii baada ya kufanya utafiti mdogo ambao unaonyesha kwamba watalii wengi huhitaji huduma ya mawasiliano ya simu sambamba na huduma ya mtandao pindi tu wanapofika katika hoteli mbalimbali nchini hapa hususan Zanzibar.
"Wakati watalii wanapofika Zanzibar, mara nyingi jambo la kwanza huwa wanauliza kuhusu upatikanaji wa mtandao, Wi-Fi na intaneti jambo ambalo linadhihirisha mawasiliano ya simu ni jambo la msingi kwao. Hilo limetusukuma kuanzisha huduma hii ili kurahisisha mawasiliano yao, "alisema Mkuu huyo wa Zantel-Zanzibar.
Alisema laini hiyo mpya itamzawadia mteja dakika 10 za kupiga Zantel kwenda Zantel, dakika 10 za kupiga zantel kwenda mitandao mingine na dakika 5 kwa simu Uhispania Ufaransa, Italia, Denmark na Marekani.
Pia laini hizo mpya zitampa mteja GB 4 kwa ajili ya intaneti kwa mwezi ambapo kitakapokwisha mteja anaweza kuchagua vifurushi vya muda wa maongezi na data kwa ofa zinazotolewa na Zantel.
Aliongeza kwamba kila laini ya simu kwa huduma hii, itauzwa Dola 10 za Marekani au Shilingi ya Kitanzania inayoendana na thamani hiyo ya fedha. Na watumiaji watapaswa kufuata hatua za kujisajili zilizo chini ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).
Akitoa taarifa nyingine kwenye mkutano huo mjini Zanzibar, alisema Zantel inalipa kodi ya shilingi bilioni 2 Serikalini kwa kila mwezi na kiasi cha Shilingi  bilioni 24  kwa mwaka.
Aliongeza kuwa Sekta ya utalii inachangia kwa asilimia 25 hadi 27 kwenye bajeti yam waka Zanzibar na akasisitiza kuna haja ya kuimarisha zaidi sekta hiyo ya utalii ili kuongeza watalii wengi kutembelea Zanzibar.
Mawasilino na Vyombo vya Habari:
Rukia Mtingwa
Tovuti: www.zantel.com

KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU ZANTEL
Zanzibar Telecom PLC (Zantel) ni kampuni inayotoa huduma za Mawasiliano nchini Tanzania pia ikitoa ofa za huduma za mawasiliano kwa njia ya simu za kimataifa.
Pia inatoa huduma ya mtandao kupitia mfumo wake wa GSM, 3G na 4G. Zantel imekuwa ikihudumia wateja wengi wanaoongezeka kwa kasi jambo ambalo limethihirisha ubora wa huduma zake, huku wakipata huduma bora zaidi kupitia mfumo wa   Best & Fastest Wireless Internet Service inayotolewa nchini Tanzania.
Zantel imepata tuzo mbalimbali kutokana na ubora wa huduma zake na uvumbuzi kwenye teknolojia ya kisasa. Miongoni mwa tuzo hizo ni- GSMA M - Health Award.
Matarajio ya ZANTEL ni kuiunganisha dunia na teknolojia ya kisasa ambayo itawawezesha watu kuwa wa mbele kupata taarifa.
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu: www.zantel.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.