Habari za Punde

Zanzibar Heroes waendelea kujifua, Selembe Pekee kafika kutoka Ligi Kuu Bara

 Mchezaji wa Zanzibar Heroes Suleiman Kassim "Selembe" akijifua 
Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakiwa katika mazoezi leo Uwanja wa Amaan


Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Ikiwa leo ni siku ya nane tangu kuanza mtizi Kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kinaendelea na mazoezi yake kujiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017 huko nchini Kenya.

Mazoezi hayo yanayosimamiwa na kocha mkuu wa kikosi hicho Hemed Suleiman (Morocco) yanaendelea kila siku kuanzia saa 2:00 za asubuhi katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja ambapo kocha huyo ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 30.

Mpaka sasa wachezaji waliyoanza mazoezi ni wale ambao vilabu vyao vya Unguja na Pemba huku ikiwa bado wachezaji wanaocheza ligi kuu soka Tanzania Bara hawajafika isipokuwa mmoja tu Suleiman Kassim (Seleembe) kiungo mshambuliaji wa Majimaji ya Songea.

Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Nassor Mrisho (Okapi), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni), Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi) na Mbarouk Marshed (Super Falcon) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto) pamoja na Mwalimu Mohd (Jamhuri).

Wachezaji ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania bara ambao bado hawajajumuika na wenzao ni Walinzi Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar) pamoja na washambuliaji Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).

Kiungo mshambuliaji Feisal Salum (JKU) nae bado hajajiunga na wenzake kufuatia kuwepo kambi ya timu ya Taifa ya Vijana Tanzania wenye umri chini ya miaka 23 Kilimanjaro Warriors.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.