Habari za Punde

Yanga yatinga Nusu Fainali Mapinduzi Cup Yaifunga Mlandege 2-1


Na Salum Vuai, ZANZIBAR


YANGA SC imeendeleza ubabe katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Taifa ya Jang’ombe usiku huu katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi tisa baada ya mechi tatu, sawa na vinara wa kundi hilo, Singida United ambao wapo juu kwa wastani mzuri zaidi wa mabao.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Rashid Farhan aliyesaidiwa na Ame Abdallah na Yussuf Abdallah, Yanga ilimaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza kwa bao 1-0.

Na bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Ibrahim Ajib Migomba dakika ya 45 na ushei, akimalizia mpira uliotemwa na kipa Ahmed Ali Suleiman kufuatia shuti la mshambuliaji mwenzake, Yohanna Oscar Nkomola.



Pamoja na Yanga kuondoka uwanjani wa kiwa wanaongoza kwa bao hilo la Ajib, lakini timu hizo zilishambuliana kwa zamu na dakika ya 36 kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali la Samir Yahya. 



Dakika sita baada ya kuanza kipindi cha pili, Taifa Jang’ombe ilipata pigo baada ya kipa wake namba moja, Ahmed Ali Suleiman kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Juma Machano.

Yanga wakafanikiwa kupata bao la pili dakika ya 60 mfungaji Nkomola, aliyemalizia pasi ya Raphael Daudi. Ajiba akatajwa mchezaji bora wa mechi baada ya mchezo huo.

Singida United watateremka tena uwanjani kesho kumenyana na JKU Saa 10:30 jioni, kabla ya mechi kali ya Kundi A kati ya Simba SC na Azam FC Saa 2:15 usiku, wakati Yanga itarudi uwanjani Jumapili kumenyana na Zimamoto FC.

Mechi za makundi zitakamilishwa Jumatatu, Simba SC wakimenyana na URA Saa 10:30 jioni na Yanga SC na Singida United Saa 2:15 usiku, kabla ya Nusu Fainali kuchukua nafasi Januari 10.

Kikosi cha Taifa Jang’ombe kilikuwa; Ahmed Ali Suleiman/Juma Machano51, Ali Mkadam, Muharam Issa, Ali Maarifa, Ibrahim Abdallah, Samir Yahya, Ahmad Mkubwa/Juma Khamis dk33/Baraka Ushindi dk57, Mohammed Salum, Yussuf Seif, Said Salum/Ali Khamis Fakhi dk80 na Ilyasa Suleiman.

Yanga SC; Ramadhani Kabwili, Pato Ngonyani, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Said Mussa/Yussuf Mhilu dk86, Raphael Daudi/Pius Buswita dk86, Yohanna Nkomola/Juma Mahadhi dk86, Ibrahim Ajib na Geoffrey Mwashiuya/Baruan Akilimali dk75

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.