TAARIFA KWA UMMA
Dar es Salaam, 20 Februari, 2018
MATOKEO YA UCHUNGUZI
KUHUSU KAULI YA ASKOFU
ZACHARY KAKOBE
Kufuatia
kauli iliyotolewa na Askofu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible
Fellowship katika mahubiri ya Ibada ambayo alisema kuwa “Yeye ana pesa kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”,
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanya uchunguzi ili kubaini usahihi wa
kauli hiyo.
Yafuatayo ni mambo
ambayo yalibainika baada ya kufanyika uchunguzi kuhusu kauli ya Askofu Zachary
Kakobe;
1.
Askofu
Zachary Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya fedha hapa
nchini. Aidha uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi
wakuu wa akaunti za kanisa (signatories) zilizopo katika benki ya NBC zenye
jumla ya kiasi cha shilingi 8,132,100,819.00, kiasi hiki cha fedha kimetokana na
sadaka, zaka na changizo ambazo zinatolewa na waumini wa kanisa tajwa hapo juu,
hivyo kwa mujibu wa Sheria hakitozwi kodi.
2.
Kanisa
lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00
ambazo zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza mitaji.Kodi hiyo
imelipwa baada ya uchunguzi.
3.
Kampuni
inayomilikiwa na watoto wa Askofu Zachary Kakobe ilikwepa kulipa kodi kiasi cha
shilingi 37,280,030.00 ambazo
zimelipwa baada ya uchunguzi. Kwa ujumla, kiasi cha kodi kilicholipwa kutokana
na uchunguzi huu ni shilingi 58,114,873.00.
4.
Kanisa
linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na ‘majaba’ kinyume na taratibu
za utunzaji wa fedha, lakini pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki
haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha
zenyewe na wahusika.
5.
Pia
ilibainika kwamba Kanisa halitengenezi hesabu za Mapato na Matumizi ya Fedha
kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja na sheria za usimamizi
wafedha ambayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za waumini kama vile safari
za nje ya nchi ambazo zimedhaminiwa na Kanisa lakini wanaosafiri ni Askofu na
familia yake. Vile vile fedha za Kanisa
zinatumika kujenga nyumba ya mke wa Askofu, kwa jina lake na wala si kwa jina
la Kanisa, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za Kanisa.
Aidha, wakati
uchunguzi huo ukiendelea,mnamo tarehe 24.01.2018 Askofu Kakobe aliandika barua
kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba radhi kutokana na
kauli yake ya kebehi pamoja na matamshi yake ya dharau kwamba ana pesa nyingi
kuliko Serikali.
WITO:
·
Mamlaka
ya Mapato Tanzaniainatoa wito kwa Taasisi zote za dini ambazo zinajihusisha na
shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa
sheria, kanuni na taratibu za kodi.
·
Mamlaka
ya Mapato Tanzania inazitaka Taasisi zote za kidini kufuata katiba zao ikiwa ni
pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumizi.
KAMISHNA MKUU
MAMLAKA YA MAPATO
TANZANIA
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
No comments:
Post a Comment