Makamu Mwenyekiti wa ZFA Pemba Ndg. Ali Mohammed ametangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo mbele ya Waandishi wa habari za michezo Kisiwani Pemba na kuonesha barua yake ya kujiuzulu.
Na.Abdi Suleiman -Pemba.
HATIMAE
sinema ya kujiuzulu kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA)
imeendelea, ambapo Makamu wa Rais wa ZFA Pemba Ali Mohammed Ali ametangaza
rasmi kujiuzulu wadhifa huo.
Makamu huyo ameungana na Rais wa chama hicho Ravia Idarous
Faina, Makamu wa Rais Unguja Mzee Zamu Ali na Abdull Ghani Msoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani pemba, Makamu huyo
alisema hatua hiyo imekuja baada ya jitathmini kwa kina na kuona tayari
viongozi wenzake wameshaachia ngazi nyazifa dhao.
Alisema kujiuzu kwake ni kutoa nafasi kwa viongozi wengine
watakao pata nafasi ya kukiongoza chama hicho kw aupande wa Pemba.
“Baada ya kuona viongozi wenzangu wa juu wamejuuzulu nyazifa
zao, sina budi na mimi nijuuzulu kama walivyofanya wenzangu, kuanzia tarehe hii
ya Leo 13/6/2018”alisema.
Aidha aliahidi kutoa mashirikiano kwa viongozi wapya watakao
kuja kukiongoza chama hicho, pale atakapo hutajika mchango wake kwa kuhakikisha
soka la Zanzibar linapiga hatua.
“Siku yoyote nitakayohitajika kusaidia kwa michango, mawazo au
lolote lile mimi nipo tayari kutoa michango wangu, ili kuona mpira wa Zanzibar
unasonga mbele”alisema.
Hata hivyo Makamu Ali Mohamed aliwaomba Radhi wale wote
aliowakosea, katika kipindi chote cha uongozi wake katika chama cha mpira wa
miguu Zanzibar upande wa Pemba.
No comments:
Post a Comment