Habari za Punde

Makamu wa Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal Mgeni Rasmin Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Jimbo la Kikwajuni Viwanja vya Mapinduzi Squya Michezani Zanzibar.

Makamu wa Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwasili katika viwanja vya Mapinduzi Squya Michezani akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni kushoto na kulia Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Nassor Salim Jazira, akielekea katika jukwaa kuu kuhudhuria Mashindano ya Nne ya Kuhifadhisha Qur-An Jimbo la Kikwajuni Zanzibar yaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Squya Michezani Kisonge Zanzibar.Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Abdilbaswit Hamis Hassan, akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar. Picha na Mpiga Picha Wetu

Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akizungumza wakati wa Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akimkabidhi zawadi, Salha Mohamed Khamis, baada ya kuibuka  mshindi wa juzuu tano wa  Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Saleh Nassoro Jazeera  na  Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia).
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal (watano kulia mstari wapili) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na washindi wa Mashindano ya Kusoma Kurani baada ya kuwakabidhi zawadi.Mashindano hayo yamefanyika katika Kiwanja cha Mapinduzi visiwani Zanzibar. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, akiwaaga wananchi (hawapo pichani), waliohudhuria  hafla ya  Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Saleh Nassoro Jazeera.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.