Na.Abdi Suleiman -Pemba.
HATIMAE
wajumbe kamati Tendaji ya chama cha soka Zanzibar ZFA Taifa, wamezikataa barua
za kujiuzulu kwa Viongozi wa juu wa Chama hicho Zanzibar.
Wajumbe wa kamati hiyo waliokutana leo katika ofisi ya ZFA Pemba
zilizomo uwanja wa michezo Gombani, huku kikao hicho kikiongozwa na Mwenyekiti
wake Sharif Juma Saidi.
Akizungumza na waandishi wa habari za Michezo Pemba, mwenyekiti
huyo alisema wajumbe wamezikataa barua za viongozi hao wa juu, kwa lengo la
kuepuka kadhia ambayo inayoweza kuipata hapo mbele, kutokana na timu za
Zanzibar zinatarajiwa kushiriki mashindano mbali mbali ya kimataifa.
Alisema awali kabla ya kuanza kikao hicho, walianza kwa kupitia vifungu
mbali mbali vya katiba ya ZFA ya 2010, ikiwemo kupata idadi ya wajumbe wa Upande
wa Pemba.
Alisema Pemba inawajumbe 14 na waliohudhuria katika kikao hicho
ni wajumbe 13, huku wakitumia kifungu cha 12 katika katiba hiyo ili kupata
maamuzi na kikao vya ZFA, pamoja na kusema kikao hicho kimepata Baraka kutoka
kifungu cha 12:2(ii) na kuwa halali.
“Kilichotuleta hapa ni kupitia barua ya Makamu wa Rais wa ZFA
Pemba Ali Mohamed Ali, aliyowasiliza ZFA juu ya kujuuzulu kwake Juni 13 mwaka
huu”alisema.
Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuipitia barua hiyo kwa mujibu
wakatiba ya ZFA ya 2010, suara ya 12 kifungu cha 92 kimesema bila ya kujali
sababu yoyote, mjumbe yoyote anayohaki ya kujiuzulu katika wadhifa alionao,
92:1 kimesema mjumbe hatajiuzulu mpaka apelike kwa tendaji katika ngazi
inayohusika, ndipo kifungu cha 92:2 ndicho kilichowapa nafasi ya kusikiliza
ombi la mjumbe.
“Sisi hapa hatukaja kujadili bali tumekuja kukubali ombi lake au
kukataa ombi lake la kujiuzulu wadhifa wake tu”alisema.
Aidha alisema baada ya kufikia muwafaka wajumbe waliweza kutumia
kifungu cha 36 katika katiba ya 2010 ya ZFA juu ya upigaji wa kura, ili kufikia
maamuzi ambapo maamuzi yanaweza kufikiwa kwa njia ya upigaji wa kura, (i)
upigaji wa kura utakuwa wa siri kwa kamati tendaji (ii) maamuzi yaweze
kuafikiwa na wajumbe.
Alisema upigaji wa kura hizo wajumbe 13 waliohudhuria kikao
hicho, kura mbili ziliharibuka na kura Tano ziliweza kukubali kujiuzulu kwa
makamu huyo wa Rais wa ZFA, huku kura sita ziliweza kumkatalia maamuzi yake ya
kujuuzulu wadhifa huo na wajumbe kumtaka katibu wa ZFA Taifa, kumuandikia barua
ya kurudi tena katika nafasi yake ya uongozi.
“Kutokana na maamuzi hayo ya wajumbe ya upigaji wa kura, kikao
hicho hakikuridhia kujiuzulu kwa makamo huyo” huku wakimtaka katibu Mkuu
kumuandikia barua ikizingatiwa mbele kuna hatua ya nane bora ya ligi kuu ya
zanizbar.
Wakati huo huo alisema Kamati hiyo ilikaa kikao Juni 12 ambapo
wajumbe walikuwa 10 na kora iliweza kutimia kwa kupitia barua mbili, ikiwemo ya
kujiuzulu kwa Rais wa ZAF Ravia Idarous Faina na Mkurugenzi wa Ufundi
Abdullghan Mssoma ambayo ilikwenda kwa Rais.
Alisema kura 10 ziliweza kumkatalia kujiuzulu kwa Ravia na
kumtaka katibu mkuu kumuandikia barua ya kurudi madarakani, huku Mzee Zam Ali
akiridhiwa kujiuzulu kwake kutokana na sababu mbali mbali alizozieleza katika
barua yake.
No comments:
Post a Comment