Habari za Punde

Zanzibar Kidedea Michuano ya Umiseta Mwanza

MASHINDANO ya Umisseta yanazidi kushika kasi hapa Mwanza, huku timu ya kanda ya Pemba na Unguja zikiendelea kufanya vyema kwa baadhi ya michezo.

Katika michezo iliyochezwa leo nyakati za asubuhi, mchana na jioni, timu ya riadha Kanda ya Unguja imeweza kutinga hatua ya fainali baada ya kutamba kwenye mbio za mita 100 wanaume na wanawake, ambapo walioshinda ni wanaume ni Mohamed Rashid na Omar Rashid, wanawake ni Naima Ali na Nasra Abdalla Abdalla.

Lakini kanda ya Pemba kwa upande wa riadha haikufanya vyema baada ya wakimbiaji wake kushindwa kuingia hatua ya fainali kwenye mbio za mita 100 , wakati mbio za mita 400 iliweza kushika nafasi ya nne na sita katika makundi yao.

Wakati  huo huo kanda ya Unguja imeweza kutoka na ushindi katika mchezo wa mpira wa kikapu ambapo ilicheza michezo miwili tofauti.
Mchezo wa kwanza iliweza kutoka na ushindi wa vikapu 62-13 dhidi ya mkoa wa Njombe, wakati mchezo wa pili Unguja iliishinda mkoa wa Mtwara kwa vikapu 24-23.

Mchezo wa mpira wa mikono Unguja iliweza kutoka na ushindi wa mabao 25-12 dhidi ya mkoa wa Njombe, pambano ambalo Unguja ilitawala zaidi kipindi cha kwanza, lakini ikapunguza kasi kipindi cha pili na kuwapa nafsi wapinzani kupata mabao.

Mpira wa netiboli timu Unguja imeendelea kuchemsha katika michezo yake, baada ya kupokea kichapo cha mabao 42-31 kutoka kwa mkoa wa Mara, matokeo ambayo yanaiweka nafasi finyu Unguja kuweza kuiongia hatua ya robo fainali.

Lakini pia kanda ya Unguja imeweza kufanya vyema katika mchezo wa mpira wa Meza (Table tennis), ambapo michezo miwili ilipigwa, mchezo wa kwanza mchezaji Sultani Suleiman alishinda kwa seti 2-1 dhidi ya Mkoa wa Manyara, wakati mchezo wa pili Mwanajuma Bakar alishinda kwa seti 2-0 dhidi ya Manyara.

Mpira wa mchezo wa Wavu Unguja ikaendelea kufanya vibaya baada ya kufungwa tena seti 3-0 na mkoa wa Mara, hivyo hadi sasa kupoteza michezo mitatu.

Kwa upande wa soka timu ya Pemba imefanikiwa kuwachapa Dodoma 1-0 huku ikiendelea kuongoza kundi lake B kwa kujikusanyia alama 12 baada ya kushinda michezo minne na kupoteza mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.