Habari za Punde

Mfumo Mpya wa Malipo Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuboresha Huduma kwa Wananchi.

Mkufunzi wa mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Augustino Manda (aliyesimama) akitoa maelezo ya awali ya mafunzo hayo kwa Maafisa Manunuzi kutoka Halmashauri za Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Arusha na Manyara , leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa malipo Epicor  toleo Na. 10.2 ambao ni Maafisa Manunuzi kutoka Halmashauri za Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga,  Arusha na Manyara wakifuatilia mafunzo hayo yaliyoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), leo Jijini Dodoma.

Mkufunzi wa mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Augustino Manda (aliyesimama) akitoa maelekezo ya namna ya kutumia mfumo huo kwa Maafisa Manunuzi kutoka Halmashauri za Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga,  Arusha na Manyara, leo Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.