Zantel inapenda kuwataarifu wateja wake, wadau na jamii kwa ujumla kuwa imesimamisha mauzo ya laini zake za simu kwa mawakala wake wakuu kuanzia sasa.
Maamuzi haya magumu yamechukuliwa kutokana na tuhuma za kuwepo kwa matumizi kuanzia wa Zantel.
Zantel imedhamiria kuzingatia na kusimamia sheria zote na kanuni zote pamoja na kufuata viwango vya juu vya maadili na kampuni haitavumilia vitendo vyovyote vya udanganyifu kupitia mtandao wake. Tunashirikiana na Mamlaka za serikali kushughulikia tuhuma za makosa haya na tutachukua hatua zote ili kuepusha hatari zaidi katika suala hili.
Zantel inawahakikishia wateja wake kuwa hakuna madhara kwenye huduma zinazotolewa kwao na wateja wanaweza kuendelea kutumia huduma na kununua laini za simu katika maduka ya Zantel na mawakala wake usajili wa laini za Zantel.
Imetolewa na uongozi wa Zanzibar Telecommunications PLC.
Maisha : Rais Dkt. Samia Ashiriki Ufunguzi wa Hema la Ibada ya Kanisa la
Arise and Shine Kawe Jijini Dar es Salaam
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan akisogeza kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi na kukata
utepe Ufu...
5 hours ago
No comments:
Post a Comment