Habari za Punde

Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Tamasha la Utalii Zanzibar, Baada ya Kuzinduliwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombe akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Tamasha la Utalii Zanzibar baada ya kuizundua Kamati hiyo kwa ajili ya maandalizi ya Tamasha Hilo Kubwa kufanyika Zanzibar kwa Mara ya Kwanza na kuhudhuriwa na Wadau wa Utalii Duniani. Linalotarajiwa kufanyika katika mwazi wa Octoba katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar kwa maonesho ya Utalii na Mahoteli.
Wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Utalii Zanzibar wakifuatilia mazungumzo yao na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Mahmoud Thabit Kombe, akizungumza na lengo la Tamasha hilo kuitangaza Zanzibar katika Sekta ya Utalii Duniani.
Wajumbe wa Kamati za Tamasha la Utalii Zanzibar wakifuatilia Mkutano huo na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar. Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Tanzania Ndg. Edwin N Rutageruka, ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya Tamasha la Utalii Zanzibar akizungumza wakati wa mkutano huo wa Uzinduzi wa Kamati hiyo uliofanywa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar. Mhe. Mahmoud Thabit Kombe katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Utalii Zanzibar Dkt Vuai Iddi Lila, akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombe kuaza kazi rasmin ya maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi wa Oktoba 2018, katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar. 

Wajumbe wa Kamati za Tamasha la Utalii Zanzibar wakifuatilia Mkutano wao wa kwanza baada ya kuzinduliwa Kamati hiyo na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.