Habari za Punde

MKUU MPYA WA WILAYA YA HAI,LENGAI OLE SABAYA AAPISHWA KILIMANJARO

Mkuu mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akila kiapo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira (hayupo pichani) ,Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akitia saini katika karatasi ya Kiapo mara baada ya kuapa kushika nafasi ya Ukuu wa wilaya ya Hai.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira (kushoto) akitia saini katika karatasi ya kiapo,mbele yake ni Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akishuhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya katiba ya Jamhuri ya Muungano muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya Ilani ya Chama cha Mapinduzi muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipena mkono na Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya muda mfupi baada ya kuapishwa.kushoto kwa Warioba ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga ,Aaron Mbogho,anaye mfuatia ni Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Senyamule na mwishoni Mkuu wa wilaya ya Siha ,Onesmo Buswelu.
Zoezi la kuapishwa kwa Mkuu huyo mpya wa wilaya ya Hai ,limeshuhudiwa pia na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi(Kushoto) na kulia ni Mwakilishi wa kamisha wa sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma,Rehema Mwakajube.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya za mkoa a Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro pia walikuwepo kushuhudia tukio hilo.
Mwakilishi wa kamisha wa sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma,Rehema Mwakajube.
Baadhi ya familia ya Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,pia walikuwepo kushuhudia tukio hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza mara baada ya kuapishwa .
Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya ya Hai na mkoa wa Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira leo amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.

Hafla fupi ya kuapishwa kwa mteule huyo wa Rais Magufuli imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,Wakurugenzi,Makatibu tawala wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na ndugu na marafiki wa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Hai.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.