Habari za Punde

Mwanafunzi Bora Zanzibar Kutoka Skuli ya Sekondari Lumumba Fahad Rashid Salum.

HONGERA FAHAD, HONGERA LUMUMBA

Fahad Rashid Salum    mwenye umri wa miaka 20 ni mwanafunzi ambaye ametuletea faraja mpya kwa Skuli ya Lumumba pamoja na Wazanzibari wote baada ya kuweza kuirudisha hadhi ya Skuli hii kwa kupata Division One ya point 3, akiwa na alama "A" katika masomo ya Mathematics, Physics na Chemistry na kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa kwa masomo ya Sayansi.

Mapema hivi karibuni, tarehe 7 Julai 2018 katika mahafali ya Kidato cha sita ya Skuli ya Lumumba , Fahad alizawadiwa kuwa mwanafunzi bora wa masomo ya sayansi, huku akikwapua zawadi ya mwanafunzi bora wa Advance Mathematics na mwanafunzi bora wa Physics.

Kabla ya Kujiunga Lumumba, Fahad alipasi mchepuo kutoka Skuli ya msingi ya Mtopepo mnamo mwaka 2012.

Mwaka 2015, Fahad alitokea mwanafunzi wa pili bora kitaifa kwa Zanzibar kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambaye alipata Division One ya point 10.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.