Habari za Punde

NEC YATEUA MADIWANI NANE (8)WANAWAKE WA VITI MAALUM

21/7/2018.  DAR ES SALAAM
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya uteuzi madiwani nane (8) wanawake wa viti maalum kujaza nafasi wazi  za madiwani katika halmashauri nane (8) za Tanzania bara.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema kuwa uteuzi huo umefanyika baada ya NEC kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi wazi za Madiwani wanawake wa Viti Maalum
Jaji Kaijage amesema kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ilipokea taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani wanawake wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufuatia walioteuliwa awali kufariki dunia au kujiuzulu.
Amewataja madiwani hao kuwa ni Ndugu Ajira Rajabu Kalinga(CCM-Halmashauri ya Wilaya ya Songea), Ndugu Mary Kazindogo Mbilinyi (CCM-Halmashauri ya Wilaya ya Makete), Ndugu Zainab Abdi Mabrouk (CCM-Halmashauri ya Manispaa ya Kongwa).
Wengine ni Ndugu Restuta Aloyce Gardian (CCM-Halmashauri ya Wilaya ya Muleba), Ndugu Siglinda Sylvesta Ngwega (CCM-Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro), Ndugu Zena Saadi Luzwilo (CCM-Halmashauri ya Mji Kahama), Ndugu Neema Michael Massawe (CHADEMA-Halmashauri ya Wilaya ya Monduli) na Ndugu Teodola Myula Kalungwana (CHADEMA-Halmashauri ya Manispaa ya Iringa).
Mwisho


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.