Habari za Punde

Resi za Ngalawa Zanzibar Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF Ufukwe wa Shangani Zanzibar.


Wananchi wa Visiwani Zanzibar wakiwa katika ufukwe wa pwani ya Shangani Zanzibar wakifuatilia Resi za Ngalawa zilizoanzia katika eneo hilo. Ikiwa ni shamrashamra za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF.
Washindi wa kwanza wa Resi za Ngalawa za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, Ngalawa iliyodhaminiwa na Kampuni ya Rahisi yenye jina Fimbo kutoka ikiongozwa na Nahodha Suleiman Ali, imetokea ya kwanza katika Resi za Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF. ikiwasili katika ufukwe wa pwani ya Shangazi Unguja baada ya kumaliza mashindano 

Washindi wa Pili wa Resi za Ngalawa za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, Ngalawa iliyodhaminiwa na Kampuni ya ZATI yenye jina Cherekwe kutoka Nyamazi Unguja,ikiongozwa na Nahodha Saddi Ali ,imetokea ya Pili,katika Resi za Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF. ikiwasili katika ufukwe wa pwani ya Shangazi Unguja baada ya kumaliza mashindano 

Washindi wa Tatu wa Resi za Ngalawa za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, Ngalawa iliyodhaminiwa na Taasisi ya WIOMSA yenye jina Ndio Hii kutoka Nyamazi Unguja,ikiongozwa na Nahodha Saddi Ali ,imetokea ya Tatu,katika Resi za Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF. ikiwasili katika ufukwe wa pwani ya Shangazi Unguja baada ya kumaliza mashindano 
Wananchi wakichukua picha kupitia simu zao wakati wa mashindano ya Resi za Ngalawa za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF. wakati zikiwasili katika ufukwe wa pwani ya shangali Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini Unguja Rajab Ali Rajab akitowa nasaha zake kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Resi za Ngalawa za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF. Akiwa na Meneja wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar Daniel Nyalusi. 
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini Unguja Mhe. Rajab Ali Rajab akimkabidhi zawadi yake Nahodha wa Ngalawa ya Fimbo Ndg. Suleiman Ali. baada ya ngalawa yake kuchukua nafasi ya kwanza wa Resi hizi za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini Unguja Mhe. Rajab Ali Rajab akimkabidhi zawadi ya Dau Nahodha wa Ngalawa ya Fimbo Ndg. Suleiman Ali. baada ya ngalawa yake kuchukua nafasi ya kwanza wa Resi hizi za Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini Unguja Mhe. Rajab Ali Rajab akimkabidhi zawadi yake Nahodha wa Ngalawa ya Chereko kutoka Nyamazi Ndg.Saddi Ali, kwa kushika nafasi ya Pili ya Resi za Ngalawa  Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini Unguja Mhe. Rajab Ali Rajab akimkabidhi zawadi yake Nahodha wa Ngalawa Ndi Hii kutoka Nyamazi Ndg.Sururu Hassan, kwa kushika nafasi ya Tatu ya Mashindano ya Ngalawa ya Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.