Habari za Punde

Mkutano wa 38 wa SADC wamalizika wamalizika mjini Windhoek, Namibia

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye siku ya mwisho ya mkutano wa 38 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo mjini Windhoek Namibia ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha Agosti 2018 hadi Agosti 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini moja kati ya nyaraka nne za kisheria ambazo  ni Tamko la Kutokomeza Malaria katika ukanda wa SADC, Itifaki ya Kulinda Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina mpya za Mbegu za mimea katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, itifaki ya ajira na kazi pamoja na Maboresho ya Katiba inayosimamia masuala ya kamati Ndogo ya Wakuu wa Polisi katika Organ. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.