Habari za Punde

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma Aongoza Ujumbe wa Zanzibar Katika Mkutano wa 49 Mabunge Wanachama Nchi za Jumuiya ya Madola Unaofanyika Nchini Botswana.

Makamu wa Rais wa Botswana Mhe Slumber Tsogwane akipata picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji na viongozi mashuhuri huko Gaborone Botswana.  
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akibadilishana mawazo na Mhe Maria Ndilla Kangoye ambae ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Kanda ya Afrika na pia Mbunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. 
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Mabunge wanachama wa nchi za Jumuiya ya Madola tawi la Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said pamoja na Katibu wa tawi hilo ambae pia ni katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Msellem wakisikiliza mada zinazojadiliwa. 
Mwenyekiti wa kamati tendaji ya nchi wanachama wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola Mhe Simai Mohammed Said akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza kutoka Rodrigues Regional Assembly Mauritius Mhe Marie Pricie Anjela Speville, katikati ni Makamu wake Mhe Ramdally Jean Rex. 
Balozi wa Nigeria nchini Botswana HE Moses I. Adeoye (kati) akifurahia jambo pamoja na Naibu Spika Mhe Mgeni Hassan na Mhe Simai Mohammed Said. Kulia wa pili ni Mhe Kabiru Mjinyawa Spika wa Jimbo la Adamawa huko Nigeria. 

Maspika kutoka (kushoto) Uganda, Mauritius, Kenya na Zanzibar wakizungumza na wanachama wa mabunge yao katika kikao cha ndani za nchi za Afrika Mashariki. 
Wajumbe wanachama wa mabunge ya nchi za jumuiya ya madola kutoka kanda ya Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Seychelles, Mauritius, Rwanda na Zanzibar wakisikiliza mada zinazozungumziwa katika mkutano huo.  
Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi (MB) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Tawi la Zanzibar  Mhe Simai Mohammed Said, kushoto Mjumbe wa Kamati Tendaji Afrika, Mbunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Maria Ndilla Kangoye.  
Kikundi cha sanaa kinachoitwa "Cultural Ensemble" wakitoa burudani watika Mkutano huo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.