Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda ndege ya Rais tayari kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulikwenye kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu Philip Mangula akiwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) Mhe. John Momose Cheyo wakiwa ndani ya ndege ya Rais kabla ya kuondoka kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018. Katika safari hiyo viongozi hao wanafuatana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) ambaye atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli(Picha na Ikulu)
JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI
YA RAIS,
IKULU,
1
BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Mstaafu wa Awamu
ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi hii kuelekea
Harare nchini Zimbabwe ambapo anakwenda Kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa
Jamhuri ya Zimbabwe Mhe.Emmerson Mnangagwa zinazofanyika leo tarehe 26 Agosti,
2018 katika uwanja wa michezo waTaifa Mjini Harare.
Akizungumza kabla ya
kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini DSM, Mhe.Rais Mstaafu Kikwete ambaye amefuatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(Bara) Ndg. Philip Mangula na Mwenyekiti wa Chama cha UDP Ndg. John Cheyo , amesema Tanzania na
Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kindugu kwani katika
kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya wananchi wake
waliwahi kuishi nchini Tanzania, husasani wanachama wa Chama cha ZANU PF,
na kupata mafunzo hapa nchini.
‘’Baadhi ya wanajeshi
wetu wameshiriki pamoja na wanajeshi wa Zimbabwe katika harakati za ukombozi wa
Zimbabwe na ndio maana kwenye Jeshi letu kuna medani ya Zimbabwe’’ amesema Rais Mstaafu
Kikwete.
Rais Mnangagwa anaapishwa leo kuongoza taifa la Zimbabwe baada ya
kushinda katika uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 30 Julai, 2018
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Agosti, 2018
No comments:
Post a Comment