Habari za Punde

Bonaza la Michuano ya Kuadhimisha Miaka 61 ya Timu Kongwe ya Ujamaa Zanzibar Linaendelea Leo Kwa Mchezo wa Taifa ya Jangombe na Gulioni City Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Na.Mwandishi Wetu. 
Michuano ya Tamasha la Timu ya Kongwe ya Ujamaa linaendelea leo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar saa kumi kwa kuzikutanisha Timu za Taifa ya Jangombe na Gulioni City, 
 Bonaza hilo linalozishirikisha Timu Nane za Wilaya ya Mjini Unguja liliaza juzi kwa mchezo wa ufunguzi uliozikutanisha Timu za Kundemba na Rastazoni  katika Uwanja wa Amaan, katika mchezo huo Timu ya Kundemba imeyaaga mashindano hayo kwa kutolewa kwa penenti na Timu ya Rastazoni.

Timu ya Gulioni City inashiriki ligi ya Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja itashukwa uwanja leo kwa kumenyana na Timu ya Taifa ya Jangombe iliokuwa tishio katika Ligi Kuu ya Zanzibar na kutowa upinzania kwa timu shiriki za ligi hiyo. Msimu uliomaliza jana wa Ligi Kuu ya Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshuka daraja 

Mchezo huo utakuwa na upinzani wa hali ya juu kila timu ikita kushinda ili kusonga mbele kulitowa kombe hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.