Habari za Punde

Eneo ambapo wanaume hukata ngozi zao ili zifanane na za mamba

Mwananchi akionesha michoro ya mwili wa mamba mgogoni katika mgogo wake baada ya kuchororwa katika mwili mfano wa mamba.
Nchini Papua New Guinea, sehemu ya mashariki ya kisiwa hicho cha pili kwa ukubwa duniani, asilimia 80 ya watu huishi vijijini na wengi sehemu zilizotengwa ambazo zina mawasiliano madogo na dunia. Hapa jinsi Mark Stratton aligundua ni kuwa tamaduni za jadi bado zinatumika.
Nyumba za kiroho au Haus Tambaran kando na mto Sepik kaskazini mwa Papua New Guinea ambapo misimu hutambuliwa kama wanyama.
Katika moja ya matambiko ya zamani zaidi duniani, wanaume wa Sepik migongo yao na mabega hukatwa kwa wembe na kuacha alama kubwa baada ya kupona kufanana na ngozi ya mamba.
Watoto wa kiume huletwa na wajomba kwenye nyumba za misimu kukatwa. Shughuli hii huchukua saa moja au masaa mawili hivi.
Moja ya eneo la Nyumba ya mizimu hutumika kwa kuombea. 
Ukiangalia miili ya wanaume iliyokatwa unaweza kuhisi machungu waliyopitia.
Watoto wengine hupoteza fahamu kutokana na uchungu wanapokatwa. Wanaume hucheza zumari na vidonda hufunikwa kwa mafuta ya mti na udongo mweupe wa mtoto kuvikinga kutona na uchafu.
"Baada ya kukatwa vijana hao wa kiume wanaweza kuishi kwenye nyumba za misimu wakijifunza mbinu tofauti za maisha kutoka wa wanaume wengine. Wanatapa ujuzi kuhusu misimu ya kijijini, jinsi ya kuvua samaki na jinsi ya kuwasaidia wake na familia," anasema Malingi.
Ninauliza kuhusu ni vipi mamba walikuja kuwa ishara ya misimu huko Sepik. "Mamba ni ishata ya nguvu, anasema Malingi. "Tunawaogopa lakini sisi hupata nguvu kutoka kwao." Ananiambia kuwa kuna imani kuwa watu wa Sepik walitoka kwa mamba na kuibuka kutoka mtoni na kutembea ardhini.
Vijiji vingi viko mbali na vigumu kufikika na havina mawasiliano na dunia. Wanaishi kwa kula chakula kinachojulikana kama Sago na samaki. Mimea wanayotegemea kwa minajili ya kifedha ni miwa. Nguruwe hufugwa kwa sherehe kama za kafara na kama pesa za kutatua migogoro.
Mto Sepik
Hata hivyo tamaduni hiyo imetoweka kutoka kwa baadhi ya jamii zinazoishi karibu na mito. Eneo la Kaminimbit, safari ya nusu siku wa mashua, niliambawa kuwa ukatajia huo wa ngozi umesitishwa kutokana na ushawishi wa wa kanisa la kikiristo. Baada ya utawala wa Ujerumani mwaka 1885 eneo la Sepik lilianza kupata injili.
Mafuvu ya mamba yaliyopakwa rangi huko Kaminimbit

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.