Habari za Punde

Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amtembelea na kumfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI

 Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally, akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono wake wa kushoto.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt. Hamisi Kigwangalla akimuonesha Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally (aliyeketi katikati),  eneo la jeraha la mkono wake wa kushoto aliopata ajari hiyo ya gari Agosti 4,Mwaka huu.
 Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally (aliyeketi katikati), akiongoza dua maalum ya kumuombea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla. Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Taasisi ya MOI, Fiderisi Minja (Aliyesimama)  na Mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA, Sheikh  Yusuph Hassan Tonge (aliyeketi).
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA, Sheikh  Yusuph Hassan Tonge mapema leo Agosti 4,2018 alipotembelewa katika wodi ya Taasisi ya MOI.Katikati anayeshuhudia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally.
Picha na Andrew Chale.


Na Andrew Chale
Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh, Abu Bakari Zuberi, amemtembea na kumuombea dua maalum Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara.
Mufti, Sheikh Zuberi  aliambata na Mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA, Sheikh  Yusuph Hassan Tonge ambapo kwa pamoja wameweza kuendesha dua maalum ili kupona haraka majeraha yake.
“Nimetoka Makka kwenye hijja tumekuombea dua. Nimerejea nikaona nije kukuona na pia kukuombea dua ili upone haraka.”  Alisema Mufti, Sheikh Zuberi.
Mbali na dua, pia Mufti, Sheikh Zuberi ameweza kumpongeza Dkt. Kigwangalla kwa juhudi zake za kazi katika Wizara yake hiyo.
Aidha, Dkt. Hamisi Kigwangalla amemshukuru Mufti Mkuu, Sheikh Zuberi  pamoja na BAKWATA kwa kuendelea kumuombea dua ambapo pia aliwaeleza kuwa kwa sasa hali yake inazidi kuimarika huku akisubiria ripoti za Madaktari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Taasisi ya MOI, Fiderisi Minja ambaye aliwapokea wageni hao, amesema kuwa Madaktari Bingwa na Wauguzi wanaendelea kutoa tiba bora kwa wagonjwa wote wanaofika kufanyiwa tiba katika taasisi hiyo.
Dkt. Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.