Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimtambulisha Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage (kulia), kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman (kushoto), baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kulia) akimkabidhi zawadi ya Kalamu yenye namba ya dharura 114, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman (kushoto), alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam jana tarehe 14/09/2018. Wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman, akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam jana tarehe 14/09/2018. Wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili.
Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru)
Diwani Athuman jana katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni
kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili.
Katika
ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye,
alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) na kumuahidi ushirikiano
katika kulijenga Taifa.
Vilevile
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru)
Diwani Athuman amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha
shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa
Jeshi hilo.
“Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa
kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana”
alisema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini
(Takukuru) Diwani Athuman.
No comments:
Post a Comment