Habari za Punde

Mafunzo ya Makocha Kwa Timu Shiriki Michuano ya Ligi Kuu ya Zanzibar Kwa Msimu wa 2018/2019.

Kamati Teule ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na Kamati ya Makocha wameandaa kozi ya Makocha (Refresher Course) kwaajili ya kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2018-2019 ambapo zaidi ya makocha 35 wakitarajiwa kushiriki.
Kozi hiyo itaanza Kesho Jumatatu Oktoba 1 hadi Alhamis ya Oktoba 4, 2018 ambayo itahusisha Makocha wa Daraja la Pili Taifa, la Kwanza na Ligi kuu ambapo inatarajiwa kuanza saa 2:30 za asubuhi katika Ukumbi wa V.I.P Uwanja wa Amaan ambapo lengo la Mafunzo hayo ni kuwapiga msasa Makocha hao kujiandaa na msimu mpya.
Mkufunzi wa Kozi hiyo anatarajiwa kuwa Abdulghani Msoma  huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya ZFA Mwalim Ali Mwalim.
Tumezungumza na Msemaji wa kamati teule ya ZFA Abubakar Khatib Kisandu alikuwa na haya kuhusu kozi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.