

Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina kulia akimlaka Mkuu wa
wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati alipofika ofisini kwake kwa
mazungumzo kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika
sekta ya uvuvi
inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani ikiongozwa na Mh. Zainab Abdallah kwa
ushirikiano na Ofisi ya Mbunge imefanya ziara ya kikazi makao makuu ya
nchi mkoani Dodoma ikiwemo kukutana na kuwa na kikao na Waziri wa
Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina na kufanikisha changamoto na
utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na
kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.
Akizungumza baada ya kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu
Abdallah alisema kikao hicho kilihusisha agenda nne kubwa muhimu kwa
ukombozi wa sekta ya Uvuvi wilayani Pangani ikiwemo Upatikanaji wa
mashine ya Storage (Compressor) na Jokofu kwa ajili ya kuhifadhi mazao
ya baharini kwa ajili ya soko kubwa la Samaki Pangani Mashariki ambalo
ujenzi wake umefanikishwa na mapato ya ndani ya halmashauri.
Hatua hiyo imepelekea Waziri Mpina kuwapongeza kwa jitihada za awali
na kuahidi kuwa Wizara yake itatoa fedha ili jokofu na compressor
vipatikane mara moja na soko lianze kufanya kazi.
Alisema kuelekea utekelezaji wa kampeni ya “VIJANA NI WAKATI WETU”
iliofanyika Wilaya ya Pangani; sekta ya uvuvi ndio iliongoza kwa
uandikishaji wa Vijana wengi.
Hivyo pia Mkuu huyo wa wilaya aliwasilisha ombi la kupata Engine
za Boti za uvuvi kwa ajili ya vikundi vya vijana walio tayari
kujiajiri na kujipatia kipato kupitia sekta hii. Wizara kupitia ruzuku
yake itagharamia 40% na 60% igharamie halmashauri husika.
Ambapo kufuatilia ombo hilo Wizara hiyo imeridhia kutoa Engine
za kutosha kwa vijana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Halmashauri
itatumia mfuko wa vijana na mfuko wa Jimbo kufanikisha upatikanaji wa
Engine hizi ili vijana wapate vifaa hivi vya kisasa na utaratibu
utawekwa kupitia Idara ya Vijana ya wilaya juu ya usimamizi na
mafunzo. Hii ni ishara ya ukombozi kwa vijana wa Pangani.
Mkuu huyo wilaya alisema pia walizungumzia suala la kuanzishwe
kwa Chuo cha mafunzo na utaalamu kwa Sekta ya Uvuvi Pangani
ikiwa ni kuelekea kupata muarobaini wa sintofahamu ya Chuo cha KIM
kurudi mikononi mwa wananchi na kuwanufaisha zaidi ya ilivyo sasa.
Hatua hiyo ilimlazimu Waziri huyo kuamua kuunda timu ya wataalamu
ambayo itakwenda Pangani mara moja kuchunguza suala hili ili ripoti
itakayo wasilishwa aweze kuitolea maamuzi kwa maslahi mapana ya wana
Pangani.
.
Sambamba na hilo liligusiwa suala la ujenzi wa Soko la Samaki na
Dagaa Kipumbwi ambapo Waziri Mpina ameweka wazi kuwa suala hili lipo
sasa kwenye mipango ya Wizara na kilichobaki ni Utekelezaji wa haraka.
na ikumbukwe mipango ilishawekwa sawa juu ya urasimishaji wa Bandari
ya Kipumbwi.
" Sekta ya Mifugo nayo haikuachwa nyuma kwa Waziri kuhahidi
upatikanaji wa Rambo la malisho ya mifugo Pangani ikiwa ni faraja
iliopotea muda mrefu kwa wafugaji wa Pangani "Alisema.
No comments:
Post a Comment