Habari za Punde

Michuano ya Kombe la FA la Dkt. Shein, Kati ya Malindi na Pangani Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Malindi Imeshinda Bao 2-1.

 
Mshambuliaji wa Timu ya Malindi Khamis Haji ( Rais ) akimpita beki wa Timu ya Pangani wakati wa mchezo wao wa Kombe la FA la Dkt. Shein, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Malindi imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.

Katika mchezo huo uliojaa ufundi kwa kila upande wakionesha jinsi ya kumiliki mpira na kutowa mashambulizi ya kutegeana Timu ya Malindi imeandika bao lake la kwanza katika dakika 53 kupitia mshambuliaji weake Haji wa Haji. 

Vijana wa Timu ya Pangani waliaza kulisakama lango la Timu ya malindi katika dakika ya 62 ya mchezo huo kipindi cha pili waliweza kuzawazisha kupitia mshambuliaji wake Juma Makame kwa shuti la mbali nje ya boksi.

Malindi walifanya mabadiliko kwa kumuingiza mchezaji wake Syprian Benedicta na kuweza kubadilisha mchezo huo na kuweza kuongeza bao lapili na la ushindi kupitia mshambuliaji wake Khamis Haji. mchezo huo umemalizika kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya timu ya malindi na kusonga mbele katika michuano hiyo. 


 Wachezaji wa Pangani wakishangilia bao lao la kusazasha wakati wa mchezo huo.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.