Habari za Punde

Taarifa ya Zoezi la Uboreshaji wa Vitambulisho Linaloendelea Katika Maeneo Mbalimbali ya Zanzibar.

Wakala wa usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar unaendelea na zoezi la kuimarisha Taarifa za Wananchi zilizomo katika Mfumo wake wa Vitambulisho vya Uzanzibari katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt Hussein K. Shaaban amesema zoezi hilo linaendea chini ya Sheria namba 3 ya 2018.
Taarifa hiyo imefafanua kwamba zoezi hilo lilianza katika Mkoa wa Kusini Unguja siku ya tarehe 08.09.2018 na linaendelea katika Wilaya ya Mjini tangu tarehe 29.09.2018.
Amesema zoezi linahusu kuimarisha taarifa kwa wote wenye vitambulisho vya uzanzibari mkaazi pamoja na waombaji wapya na Wanaobadilisha shehia.
Akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi hilo Dkt Hussein amesema Waombaji wapya watahitaji kuwa na vielelezo vyaukaazi kutoka kwenye shehia yao mpya pamoja na vyeti vyao vya kuzaliwa.
Kwa upande wa wanaobadilisha Shehia Dkt Hussein amesema wanapaswa kuwa na Vielelezo vya kuthibitsha ukaazi wao kutoka kwenye shehia yao mpya.
Mkurugenzi Hussein amesisitiza kuwa kwa Mwananchi kuwa na kitambulisho na kuimarisha taarifa zake ni wajibu wa kisheria hivyo wananchi wote washiriki katika zoezi hilo.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.