Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli Awaapisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Skauti Mkuu wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea machache kwenye hafla ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kuongea machache kwenye hafla ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza muda mfupi baada ya kumuapisha kuwa Skauti Mkuu wa Chama Cha Skauti Tanzania. Aliyeketi ni Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe aliyemuapisha kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hafla hii imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi Rais wa Chama cha Skauti na Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia Dr. leonard Akwilapo,  Skauti Mkuu Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza, Mama Anna Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha Skauti nchini Mhe. Abdulkadir Shah na makamishna wa Skauti na Girl Guide  kwenye hafla ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi na Skauti Mkuu Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama  baada ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 20 Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.