Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Atembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo Jipya ya Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimskiliza Kaimu Mkurugenzi Tiba Dr. Fadhil Abdallah, akitowa maelezo ya Ujenzi wa Jengo Jipya la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipotembelea Mradi huo wa ujenzi wake katika eneo la Hospitali ya Kivunge Zanzibar, kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Vuai Mwinyi.

Jengo Jipya la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja likiwa katika Ujenzi wake katika eneo la hospitali hiyo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Eng. wa Kampuni ya World Class Engineering Contractars Ndg. Joshua Christopher Nyari, akitowa maelezo ya michoro ya ujenzi wa Hospitali hiyo inayojengwa katika maeneo ya Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Daktari Dhamani wa Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Tamim Hamad Said, akitowa maelezo ya michoro ya jengo jipya la Hospitali ya Kivunge kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipotembelea Mradi huo wa Ujenzi wa Hospitali hiyo katika eneo la Hospitali ya Kivunge.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar, wakati alipotembelea Mradi wa Jengo la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja. kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na kushoto Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge Dr. Tamim Hamad Said na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdallah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja, kushoto Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed, wakitembelea Mradi huo wa ujenzi wa jengo hilo katika viwanja vya Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.   
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akitowa maelezo ya Mradi huo wa ujenzi wa jengo la Hospital ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea Mradi huo, akiwa katika ziara yake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akielekezwa  na kuonesha moja ya sehemu ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Zanzibar na Dr. Fadhil Abdallah wakati akitembelea Mradi huo wa Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.wakati wa ziara yake Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.