
TAARIFA KWA UMMA
Dar
es Salaam, 31 Oktoba, 2018
Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu habari zilizochapishwa katika Gazeti la
Tanzania Daima la tarehe 26 Oktoba, 2018 toleo namba 4979 na toleo namba 4982
la tarehe 30 Oktoba, 2018 zenye vichwa vya habari “Madudu yaibuka TRA” na
“Barua za madudu TRA zavuja”. Habari inayofanana na hizi, ilisambazwa pia katika
baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikiwa na kichwa cha habari "PCCB Tanzania, to investigate the two tax collectors TRA and
ZRB".
Habari hizi zinadai kuwa, Mfumo
wa Ulipaji Kodi kwa Njia ya Kielektroniki – Electronic Revenue Collection System
(e-RCS) umezimwa na kuhujumiwa na baadhi ya Maofisa wa Serikali kwa lengo la
kujinufaisha na kuzorotesha juhudi za ukusanyaji mapato ya Serikali.
Ukweli ni kwamba, mfumo huo
haujahujumiwa wala kuzimwa isipokuwa kuna maboresho ya kiufundi ambayo
yanaendelea kufanyika ili kuhakikisha kuwa, unakidhi malengo yaliyokusudiwa.
Katika kipindi hiki ambacho
maboresho yanaendelea kufanyika, Kampuni za Simu pamoja na Benki mbalimbali zinaendelea
kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na hakuna upotevu wowote wa mapato kama
ilivyoripotiwa na Gazeti la Tanzania Daima na baadhi ya Mitandao ya Kijamii.
TRA inapenda kuuhakikishia umma
kwamba, hakuna Ofisa yeyote wa Serikali mwenye nia ya kuhujumu mfumo huo kwa lengo
la kujinufaisha na kuzorotesha juhudi za Serikali za ukusanyaji wa mapato.
Mamlaka ya Mapato Tanzania inatoa
wito kwa vyombo vya habari, wachapishaji, wahariri na waandishi wa habari kufanya utafiti
wa kina kabla ya kuandika habari na kuzingatia weledi wakati wote wanapotimiza
majukumu yao ili kuepuka upotoshaji.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Imetolewa
na:
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI
WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
No comments:
Post a Comment