Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania Mr. Hamdi M.H. Abuali,alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dk.Shein, Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar
itaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati yake na Taifa la Palestina, kwa
maslahi mapana ya watu wa nchi mbili hizo.
Amesema uhusiano
na ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo ni wa muda mrefu, tangu enzi za
muasisi wa Taifa hilo, Hayat
Yasser Arafat, ukijikita katika nyanja za kiuchumi, kijamii
na kiutamaduni.
Dk. Shein amesema
hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, alipozungumza na Balozi mpya wa Palestina nchini,
Hamdi M.H. Abuali, aliefika kujitambulisha.
Alisema Serikali
imeazimia kupanua wigo wa ushirikiano na Palestina katika nyanja za kiuchumi na
kijamii, hususan kupitia sekta za Utalii, afya pamoja na biashara zitokanazo na
kilimo.
Alisema pamoja na
Taifa hilo kupitia katika changamoto mbali mbali za kiusalama, tayari imepata
mafanikio makubwa, hivyo ipo haja kwa nchi mbili hizo kushirikiana katika suala
la mafunzo pamoja na kubadilishana wataalamu.
Dk. Shein,aliwataka
wananchi wa Palestina kujidhatiti na kuongeza juhudi katika harakati za kudai
haki yao, kwa kuamini kuwa iko siku watafanikiwa.
Nae, Balozi
Abuali alimuahakikishia Dk. Shein azma ya Taifa hilo kuendeleza ushirikiano
uliopo kati yake na Zanzibar, ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na
kijamii.
Alisema Palestina itafanya kila juhudi kuhakiksha
kunakuwepo mafungamano mema kati ya nchi mbili hizo, ili kuona sekta
zilizoainishwa zinakuwa chachu ya kuendeleza uchumi wa Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822
E-mail: abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment